Baada ya kuvunja rekodi ya usajili wa ada ya juu zaidi duniani, Paul Pogba ametaja sababu iliyomfanya akubali kusaini kuichezea Manchester United baada ya kuondoka kwenye klabu hio miaka takribani minne iliyopita.
Kupitia MUTV Pogba amesema “Man United ndio timu sahihi kwangu ambayo itanifanya nipate mafanikio niliyokuwa nayatamani siku zote na nimerudi nyumbani, najiskia kama nilipokuwa palikuwa likizo” .
Paul amesajiliwa kwa ada ya pound milioni 89 na kuvunja rekodi ya Cristiano Ronaldo na Gareth Bale aliyesajiliwa kwa pound milioni 85 kwenda Real Madrid akitokea Tottenham Hospurs.
Maoni
Chapisha Maoni