Rapper aliyekuwa member wa kundi la G Unit kabla halijavunjika, Young Buckamehukumiwa kwenda jela miezi saba.
Young Buck ’35’ Jumatano amekiri mbele ya mahakama kuvunja masharti ya kifungo cha nje chini ya uangalizi wa polisi na kuhukumiwa kurudi tena jela miezi saba.
Katika akaunti yake ya Instagram Young Buck aliomba marafiki zake wawe karibu na yeye akiwa jela.
Young Buck ambaye alikuwa akiishi maisha ya uangalizi wa polisi toka mwaka 2013 na hapa kati amekuwa akivunja masharti ya kifungo cha nje kwa kukutwa akiwa ametumia bangi kwenye vipimo vya mkojo na makosa tofauti ya fujo.

Maoni
Chapisha Maoni