'Kaburu' amesema kikosi walichokisajili msimu huu ni kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye michuano ya imataifa
Makamu wa rais wa klabu ya Simba Godfrey Nyange 'Kaburu' amesema kikosi walichokisajili msimu huu ni kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye michuano ya imataifa.
Nyange amesema, wamejipanga kuhakikisha wanatwaa taji la ligi ya Vodacom ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa waliyoipania baada ya kuikosa kuipata kwa miaka minne mfululizo.
"Ukweli tumejipanga kuhakikisha msimu huu tunatwaa ubingwa na kupata nafasi ya kuwakilisha Taifa kwenye michuano ya kimataifa," amesema Kaburu.
Kiongozi huyo amesema hadi sasa wana asilimia kubwa ya kulitimiza hilo kutokana na ubora wa kikosi chao hivyo wanataka kuonyesha mfano baada ya timu ambazo zilikuwa zikipata nafasi hiyo zilikuwa zinaishia kuwa wasindikizaji.
Amesema kwa kipindi cha miaka minne wamejfunza mambo mengi ikiwemo namna ya kuandaa timu yenye uwezo wa kupambana na kufanya vizuri kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
"Ukweli viongozi wa Simba tumedhamiria na tumejipanga hatupo tayari kuona tunaridhika kwa kutwaa ubingwa wa ligi ya Vodacom bali tunataka kutwaa bingwa wa Afrika na uwezo huo tunao," amesema Kaburu.
Simba ndiyo vinara wa ligi ya Vodacom wakiwa na pointi 55 lakini wanalazimika kupambana ili kuweza kutimiza lengo lao la ubingwa msimu huu.

Maoni
Chapisha Maoni