Ruka hadi kwenye maudhui makuu

YANGA YALAZIMISHWA SARE NYUMBANI


Sare ya 1-1, dhidi ya Zanaco, imewaweka katika wakati mgumu wa kucheza hatua ya makundi Yanga ya michuano hiyo mikubwa Afrika.
Sare hiyo imeonekana kuwamuza mashabiki wa timu hiyo kufuatia kiwango kibovu, kilichoonyeshwa na timu yao jambo lililowalazimu kumfuata kocha wao wa zamani Mdachi Hans van der Pluijm na kumwomba arudi kuifundisha timu hiyo.

Matokeo yanamaanisha Yanga watahitaji ushindi wa ugenini katika mchezo wa marudiano nchini Zambia ili kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Yanga iliyokuwa nyumbani leo ilionyesha kiwango dhaifu na kuwaacha wageni weo wakijitawala na kufanya anavyotaka ikiwapo kupoteza nafasi nyingi za mabao.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa kutoka Djibouti, Djamal Aden Abdi aliyeyesaidiwa na Hassan Yacin na Farhan Salime, hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Yanga pamoja kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao moja lililofungwa na Simon Msuva dakika ya 39, lakini muda mrefu walionekana kuhangaika uwanjani kutafuta mpira  uliokuwa miguuni mwa wachezaji wa Zanaco.

Bao hilo lilifungwa na winga machachari wa timu hiyo, Simon Happygod Msuva dakika ya 39 baada ya kuwachambua mabeki wa Zanaco kufuatia pasi nzuri ya kiungo Mzambia, Justin Zulu.

Bao hilo lilikuja baada ya Yanga kubadilisha maarifa ya kuwashambulia Zanaco, kutoka kutumia mipira ya kutokea pembeni hadi kuamua kuingia ndani ya eneo la hatari kwa kugongeana pasi.
Kwa dakika zote 30 za awali, Zanaco hawakuwa na kazi ngumu kudhibiti mashambulizi yatokeayo pembeni ya Yanga, lakini baada ya mabingwa wa Tanzania, kubadilika hali ikawa ngumu upande wake.

Pamoja na kufunga bao moja, lakini ndani ya dakika 15 za kuelekea mwisho wa kipindi cha kwanza, Yanga walikosa mabao mawili zaidi ya wazi.
Kipindi cha pili Zanaco walikuja na maarifa mapya na kufanikiwa kuziba mianya ya Yanga kupenyezeana pasi hivyo kupunguza kasi ya wawakilishi hao wa Tanzania.

Yanga ikarudi kutumia mipira mirefu ya kutokea pembezoni mwa Uwanja kujaribu kulazimisha mashambulizi langoni mwa Zanaco, lakini safu ya ulinzi ya mabingwa hao wa Zambia ilikuwa imara.
Hatimaye Zanaco wakafanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 78  kupitia kwa mshambuliaji wake Mghana, Attram Kwame aliyetumia mwanya wa mabeki wa Yanga kuzubaa kusubiri wapinzani wao watoe nje mpira kiungwana baada ya mchezaji mwenzao, Obrey Chirwa kuangushwa.

Kwame alifunga mbele ya mabeki wa kati watatu wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan na Vincent Bossou na kipa wao Deogratius Munishi ‘Dida’ baada ya krosi kutoka wingi ya kulia.
Bao hilo lilionekana kabisa kuwavunja nguvu Yanga na kutoka hapo wakaanza kucheza ili kumalizia mchezo kwa sare na si kutafuta ushindi.

Wachezaji Juma Mahadhi na Emmanuel Martyin walioingia kwa upande wa Yanga kuchukua nafasi ya Donald Ngoma na Thabani Kamusoko, walionekana kushindwa kuiunganisha timu na kuzidi kuwapa nguvu wapinzani wao Zanaco kuendelea kuwashambulia.

Matokeo hayo yanawalazimu Yanga kushinda mchezo wa marudiano ili waweze kufuzu hatua ya makundi vinginevyo huo utakuwa ndiyo mwisho wao na ndoto za kuutwa ubingwa wa michuano hiyo kwa mwaka huu licha ya kumchukua kocha Lwandamina aliyeifikisha Zesco ya Zambia nusu fainali ya michuano hiyo mwaka jana.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House

Trump: Tajiri anayetaka kuingia White House Image copyright GETTY Image caption Trump huamini sana katika kushinda Donald Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na anasema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Tayari ameidhinishwa na chama cha Republican kuwania urais baada ya kuwabwaga wapinzani wengine. Kwa wafuasi wake, mgombea huyu wa Urais kwa chama cha Republican ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Mbaguzi na mfitini Hata hivyo kwa wakosoaji wake, wanasema huyu ni mbaguzi na mfitini, muonevu mkubwa amb...

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao

Haya ndo makundi ya Wachaga na tabia zao Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja.  Wachaga hutokea maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na hua na tabia tofauti. Haya ni baadhi ya makundi ya wachaga na tabia zao. 1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji. 2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu. 3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchi...

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10. Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC. Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na Young Africans inashika nafasi ya sita. Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.