Kiongozi wa koo za Meru na mwenyekiti wa mila na jadi za Wameru Ndg Ezron Sumari amewaasa vijana wa kimeru kulinda usalama wa jamii na mali zao pamoja na kutunza nidhamu katika jamii.
Alisema hayo katika sikukuu za kusheherekea kukuza kwa vijana wa kimeru kutoka kuwa watoto na kuwa vijana mara baada ya kuingizwa jando na kufanikiwa kutoka salama na kufanikiwa kupewa rika.
Aliongoza kwa kuwakumbusha vijana kuwa kwasasa wameshakuwa hivyo wanapaswa kufanya wajibu wao wa kushiriki shughuli zote za kijamii na kiserikali pamoja na kuondoa uhalifu, kutunza nidhamu na kufanya kazi kwa kubidii
Ndg Sumari amewaasa wameru kujikita katika kukuza na kuendeleza rika tofauti na nyuma ambapo suala la rika lilisahaulika lakini kwasasa wameridhia utaratibu wa mila kamili pamoja na kuzingatia mila zao ili kukuza vijana wenye nidhamu ambao watakuwa na maadili mema na mazuri katika kulitumikia taifa.
Maoni
Chapisha Maoni